Search
Generic filters
Notifications
Clear all

Jinsi akili ya mjasiriamali inavyofikiri ukilinganisha na Mtu aliyeajiriwa  


herberth_hbt


Posts: 7
Joined: 2 years ago

Nimekuwa najiuliza hili swali kila siku au nina upekee wa kitofauti. Wajasiriamali wana kuwa na extra thinking kila wanapopita sehemu. Mjasiriamali ana angalia mambo kwa jicho la kipekee sana na ukiona mtu wa namna hii basi kaa ukijua anakabiashara sehemu flani au ana mpango wa kuanzisha biashara. 

Juzi kati niliingia kwenye mgahawa mmoja hapa mjini nikaona jinsi jamaa amejaza karibu viti vyote hadi nikawa natafuta sehemu ya kukaa kwa tabu. Ikabidi nisubiri kidogo dada mmoja amalizie nichukue nafasi yake. 

Nilipofanikiwa kukaa ghafla nikanza kuhesabu watu waliomo humu ndani takribani watu 45 na wote wameagiza chakula tofauti. 

Kila sahani ya chakula ilikuwa 10,000/= pamoja na kinywaji 2000/= jumla pale kila mtu ange tumia sio chini ya 12,000/= labda kama amekuja kunywa juice kitu amabcho sio kweli kwani kila mtu alikuwa anachakula. 

So kwa hesabu ya haraka haraka nikaona kwa muda ule jamaa alikuwa amefunga zaidi ya tshs 540,000/-. Nilipo maliza kula waiter akawa analeta bill na nikamuuliza kwa hapa huwa mnapata watu wangapi kwa siku? Akaniambia hana uhakika ila sio chini ya watu mia tatu au zaidi inategemea kwa siku.

So nikajaribu kubalance nakuweka kila mtu angeingia mule ndani anagespend shs 8000/= na kupata hesabu kuwa jamaa anapiga rough estimate ya 2,500,000/- kwa siku na 72,000,000/= kwa mwezi. 

Sasa hii figure haiwezi kuwa sahihi sana ila ni estimate tu pengine yaweza kuwa zaidi au chini ila sio mbali sana na hapo. 

 

Lesson ni kwamba ukiwa na akili ya kijasiriamali, huwa jicho lako linaangalia mambo mengi kama fursa na kutafuta njia mbadala wa kutengeneza faida. Baada ya kutoka pale niko na mpango wa kufungua restaurant maeneo kama yale.

Hii inakufanya ufanye research na kufahamu mengi zaidi kuhusu biashara hiyo.

1 Reply
tracz


Posts: 40
Joined: 2 months ago

Hahah nimependa sana hiyo kwa hiyo tuko wengi sana. Unakuta unampigia hesabu jamaa anafunga shs ngapi kama ni kubwa unawaza kuanzisha kama hiyo. Hatari sana 🤣 

Reply
Share: